Maambukizi ya corona Kenya yazidi kupanda

0

Watu wengine  727 wameambukizwa  virusi vya  corona baada ya kupima sampuli  4,913  katika muda wa saa Ishirini na nne zilzopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 78,512.

Katibu wa wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi ametangaza kufariki kwa wagonjwa 17 zaidi kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi maafa kwa 1,409.

Aidha, watu wengine 806 wamepona ugonjwa huo 701 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani na wengine 105 kwenye hospitali mbalimbali na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 52,709.

Kaunti ya Nairobi imerekodi visa 306, Kiambu 122, Kitui 38 na Uasin Gishu 33.

Wagonjwa waliolazwa hospitalini ni 1,196 huku 7,139 wakishughulikiwa nyumbani.

Wagnjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ni 51, wanaosaidiwa na mashine kupumua ni 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here