Wagonjwa 23 zaidi wameaga dunia kutokana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,203.
Akihutubia taifa katika bunge la kitaifa rais Uhuru Kenyatta amesema watu wengine 919 wameambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 66,723
Waliopona ni 414 na kufikisha idadi hiyo kuwa 44,040. Waliolazwa hospitalini ni 1,279, wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 6,102. Wagonjwa walio kwenye chumba cha watu mahututi ni 60.
Nairobi pekee imeandikisha visa 345, Mombasa 98, Nakuru 76, Kilifi 74 na Kiambu 44.