Maafa ya corona yazidi kuongezeka

0

Watu 15 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona chini ya saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 438.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema 11 kati ya wagonjwa hao walikuwa na magonjwa mengine.

Habari njema ni kwamba watu 372 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 13,867 huku visa vipya 497 vikiripotiwa na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 27,425.

Westlands imerekodi visa 31, Langata 28, Embakasi East 24, Dagoreti North 17, Kibra 15, Embakasi South 14, Kamukunji 13, Embakasi Central  sawaEmbakasi West 11, Roysambu 10, Mathare 9, Dagoreti South na  Ruaraka 8, Embakasi North & Kasarani 7 na Starehe 6.

Dkt. Mwangangi aidha amesema Nairobi imesalia kuongoza kwa kuwa na visa vingi vya ugonjwa huo wa corona ambapo kwa sasa kuna visa 16,196, Mombasa 2,154, Kiambu 1,964, Kajiado 1,514 na Machakos 971.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here