Maafa ya corona yazidi kuongezeka

0

Wakenya 267 na raia wanne wa kigeni ni miongoni mwa watu 271 waliokutwa na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema idadi hiyo imeongezeka baada ya kupima sampuli 4,019 na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 30,636.

Idadi ya watu waliopona ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 17,160 baada ya watu 208 kupona huku maafa kutokana na ugonjwa huo yakifikia 487 baada ya kufariki kwa wagonjwa watano zaidi.

Nairobi imerekodi visa 99, Kiambu & Laikipia 20, Migori na Uasin Gishu 18, Busia 12, Lamu na Samburu 11, Turkana 10, Kajiado 9, Makueni & Garissa 4, Mombasa, Machakos, Murang’a, Kisumu, Kilifi, Taita Taveta & Tana River wamerekodi visa vitatu kila mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here