Maafa ya corona Kenya yapindukia 800

0

Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona imepundikia 800 baada ya wagonjwa 8 zaidi kufariki huku visa zaidi ya 600 vikiandikishwa kwa siku ya pili mfululizo.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa anasema hii inafikisha 805 idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia sasa.

Idadi ya maambukizi nchini imeongezeka na kufika 43,143 baada ya watu 602 kupatikana na virusi hivyo.

Aidha watu 80 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 31,508.

Nairobi ingali inaongoza kwa msambao wa visa hivyo kwa kuandikisha visa 133, Nakuru & Uasin Gishu 47, Kilifi & Kisumu 46, Mombasa 44, Kericho 32, Kakamega 28, Turkana 25, Kisii 21, Machakos 20, Laikipia 13, Nyandarua & Bungoma 12, Kiambu 11, Nandi 10, Busia, Kajiado 7, Baringo na Garissa 6, Pokot Magharibi na Nyamira 5, Makueni 3, Nyeri, Embu, Siaya, Bomet na Vihiga 2, Lamu,Wajir, Samburu, Narok, Murang’a na Meru 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here