Maafa ya corona Kenya yafikia 813

0

Watu 437 zaidi wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 4,311 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hii inafikisha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 43,580.

Watu wengine 140 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 31,648 huku maafa yakifika 813 baada ya watu 8 zaidi kufariki.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatavyo; Nairobi inaongoza kwa kunakili visa 136, Nakuru 66, Kilifi 29, Kisumu 26, Uasin Gishu 21, Kericho 21,Embu 17, Busia 16, Kajiado 15, Migori 14, Machakos 14, Kiambu 9, Meru 9, Nandi 8, Bomet 6,Nyeri, Laikipia, Mombasa 5, Nyamira 3, Nyandarua, Elgeyo Marakwet, Turkana, Tharaka Nithi, Wajir, 2 Murang’a na Siaya 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here