Maafa ya corona Kenya yafikia 364

0

Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 364 baada ya wagonjwa 23 zaidi kupoteza maisha katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii ndio idadi kubwa ya maafa kuwahi kuripotiwa tangu kisa cha kwanza kudhibitishwa nchini mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Miongoni mwa waliofariki ni kijana mwenye umri wa miaka 16 hali inayoelezea wasiwasi kuhusu mkondo ambao virusi hivyo vinachukua nchini.

Aidha, watu wengine 727 wamekutwa na ugonjwa huo na kufikisha 21,363 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini Kenya kufikia sasa.

Habari njema ni kwamba idadi ya waliopona imefikia 8,491 baada ya wagonjwa wengine 254 kupona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here