Maeneo ya ibada yanafunguliwa rasmi hii leo baada ya baraza la kidini kutoa mwongozo salama wa kufuatia kuzuia maambukizi ya corona.
Miongoni mwa masharti kwenye mwongozo huo ni kwamba, ni watu mia moja pekee ambao wataruhusiwa katika ibada ambayo itadumu kwa muda wa saa moja pekee.
Maabadi pia yanatakiwa kuwa na maji na sabuni kwa waumini kunawa mikono kabla na baada ya ibada huku pia wakitakiwa kusafisha kanisa kila baada ya ibada.
Baadhi ya wahubiri kutoka kaunti ya Nakuru wakiongozwa na Jackson Maina wanasema wako tayari kuanza kuandaa ibada chini ya mwongozo uliotolewa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa dini wakiongozwa na Ustadh Mohamed Shaban wanapinga kuzuiwa kwa watu walio na zaidi ya umri wa miaka hamsini na nane kuingia mahala pa ibada na wanasema wengi wa wahubiri wamepita umri huo.
Huku baadhi wakipinga mwongozo uliotolewa, makanisa mengine yametaganza kuwa hayataanza kuandaa ibada hadi pale maambukizi ya corona yatakapopungua.
Miongoni mwa makanisa ambayo yanasema hayatafungua ibada zake ni CITAM, Parklands Baptis, Jubilee celebration center, Nairobi Chapel na makanisa ya Deliverance.
Askofu Sammy Wainaina wa kanisa la All Saints Cathedral anasema hawataanza kufanya ibada hadi pale baraza la kidini litabuni engeneza mwongozo ambao uatawafaa.