LSK yashitaki serikali kuhusu kupea KDF usimamizi wa tume ya nyama

0

Chama cha Mawakili nchini (LSK) kimewasilisha kesi ya dharura mahakamani kupinga hatua ya kuhamisha usimamizi wa tume ya nyama KMC hadi katika wizara ya Ulinzi.

LSK kupitia wakili wake Hosea Omanwa imetaja hatua hiyo ya rais Uhuru Kenyatta kama inayokiuka katiba.

Kwenye kesi yake kutaka hatua hiyo kubatilishwa, mawakili wanahoji kuwa KMC ni asasi iliyobuniwa na bunge na majukumu yake hayawezi au kuingiliwa na yeyote.

Jaji Anthony Mrima ametaja kesi hiyo kama ya dharura na kuagiza isikilizwe wiki ijayo.

Haya yanajiri siku moja baada ya maseneta wakiongozwa na Steward Madzayo wa Kilifi kutaja hatua hiyo kama ukiukaji wa sheria kwani tume hiyo inafaa kuwa chini ya wizara ya mifugo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here