LSK kumlazimisha rais kuvunja bunge

0

Kuanzia Jumatatu ijayo, chama cha Mawakili nchini (LSK) kimetishia kuwaongoza Wakenya katika kumlazimisha rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge alivyoshauriwa na jaji mkuu David Maraga.

 LSK kupitia rais wake Nelson Havi inahoji kuwa rais Kenyatta hana lingine ila kulivunja bunge na kuwatuma wabunge nyumbani kwa kushindwa kupitisha sheria kuhusu uwakilishi sawa wa jinsia katika nafasi za uongozi.

Havi anasema rais ana hadi Octoba 12 ambayo ni Jumatatu ijayo kufanya alivyoshauriwa na Maraga la sivyo watatumia kila mbinu ikiwemo kuandamana kumshurutisha kufanya hivyo.

Mawakili hao wameapa kuzuru maeneo mbalimbali nchini kuwarai Wakenya kuunga mkono kuvunjwa kwa bunge.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here