Kura ya maamuzi kuandaliwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao asema Odinga

0

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga anasisitiza kuwa taifa hili halihitaji pesa nyingi kuandaa kura ya maamuzi kurekebisha katiba.

Odinga akizungumza wakati wa kula kiapo kwa bodi mpya ya uchaguzi ya chama hicho amesema taifa hili lina uwezo wa kurekebisha katiba bila kutumia mabilioni ya pesa kama inavyodaiwa.

Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile amesema kura ya maamuzi itaandaliwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Mkondo ambao taifa hili litachukua kuhusiana na marekebisho ya katiba unatazamiwa kuamuliwa na ripoti ya mwisho ya kamati ya BBI iliyobuniwa kufuatia ushirikiano baina ya Odinga na rais Uhuru Kenyatta.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here