Kocha wa Stars Francis Kimanzi agura

0

Kocha wa timu ya taifa Harambee Stars Francis Kimanzi amejiuzulu.

Kimanzi amejiuzulu pamoja na meza yake yote ya kiufundi akiwemo Zedekiah Otieno almaarufu Zico na kocha wa walinda lango Lawrence Webo.

Mechi ya mwisho ya Kimanzi ilikua ushindi dhidi ya Chipolopolo ya Zambia walioshinda mabao mawili kwa moja ugani Nyayo mwezi huu.

Isisahaulike pia Kimanzi alikua mbioni kuiongoza Harambee stars kwenye dimba la AFCON 2021 baada ya kutoka sare na Misri jijini Cairo na Togo.

Shirikisho la kandanda nchini FKF katika taarifa kupitia kwa afisa mkuu mtendaji Barry Otieno limewatakia kila la kheri kwa jitihada zao zijazo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here