Kivumbi Senate kuhusu mswada wa ugavi wa mapato

0

Kivumbi kimeshuhudiwa katika bunge la Senate hii leowakati wa mjadala kuhusu ugavi wa mapato katika serikali za kaunti.

Juhudi za seneta wa Tharaka Nithi Profesa Kindiki Kithure kutaka mjadala tata kuhusu ugavi wa mapato kuhairishwa kwa mara nyingine kutokana na kutokuwepo kwa maseneta watatu Cleophas Malala wa Kakamega, Christopher Langat wa Bomet na Stephen Lelegwe wa Samburu kugonga mwamba.

Hii ni baada ya kuwa na idadi sawa ya maseneta waliopinga na kuunga mkono hoja hiyo.

Kiranja wa wengi katika bunge hilo Irugu Kangata alipinga hoja hiyo akisema kaunti zimesalia bila pesa kutokana na hatua ya Senate kuhairisha vikao vya kujadili mswada huo mara tisa.

Awali, waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi alikosa kufika mbele ya kamati ya bunge hilo la Senate kuhusu usalama kuelezea ni kwa nini maseneta watatu wamezuiliwa kuhudhuria vikao maalum vya bunge hilo leo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here