KIUNGO WA MANCHESTER UNITED HENRIQUE CASEMIRO ATETEWA NA MKEWE ANNA MARIANA

0

Anna Mariana ambaye ni mke wa mchezaji kiungo wa Manchester United Carlos Henrique Casemiro amtetea mume wake kufuatia kichapo cha 3-0 kutoka kwa Liverpool.

Kulingana na wachambuzi wa soka, kichapo cha Manchester United cha mabao 3 – 0 wakiwa nyumbani kwao Ugani Old Traford dhidi ya Liverpool kimehusishwa na  Casemiro, ambaye alitolewa wakati wa mapumziko.

Awali kuliibuka tetesi kwamba Casemiro aliondoka Old Trafford wakati wa mapumziko, lakini mkufunzi wa United Erik ten Hag alikanusha.Sasa mke wake Casemiro amemtetea mumewe, huku akiwakumbusha watu mataji mengi ambayo ameshinda katika maisha yake yote ya soka.

Anna Mariana alituma picha ya za mataji alioshinda kwenye ukurasa wa Instagram, huku Mbrazil huyo akiwa ameshinda Ligi ya Mabingwa mara tano pamoja na La Liga mara tatu akiwa na Real Madrid na, hivi majuzi, Kombe la F.A akiwa na Manchester United.Kisha alichapisha picha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akisherehekea na wenzake.

Kukosa kumakinika kwake Casemiro kulichangia pakubwa Liverpool kufunga mabao mawili katika dakika ya 35 na 42 kupitia mchezaji Luiz Diaz  kwenye mchezo wa Jumapili ugani Old Trafford.

Katika Mazungumzo na Sky Sports,Beki wa Zamani wa Liverpool Jamie Carragher alionyesha kusikitishwa na hali ambapo Casemiro alikuwa akikumbana nayo nje ya Uwanja.Aidha aliyekuwa beki wa zamani wa Manchester United Gary Neville amehusisha mchezo wa Casemiro wa sasa na kukosa kujiamini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here