Kioni Nyaribo wakutana kujadili azma ya urais ya Matiangi

0

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni ameandaa mkutano na kiongozi wa chama cha United Progressive Alliance (UPA) Gavana Amos Nyaribo kujadili azma ya Urais ya waziri wa zamani Fred Matiangi.

Vyama vya UPA na Jubilee vimeeleezea nia ya kuwasilisha jina ya Matiangi ambae alihudumu kama waziri wa usalama wa ndani katika utawala uliopita kama mwaniaji wao wa Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

“Majadiliano ya mapema asubuhi na Mheshimiwa Gavana Nyaribo, Kiongozi wa Chama cha UPA na Gavana wa Kaunti kuu ya Nyamira,” Kioni amesema kwenye akaunti yake ya X.

Katibu huyo mkuu amesema majadiliano yao yamejikita kwenye maswala ibuka, mustakabali wa taifa na nafasi ya matiangi katika uchaguzi mkuu ujao.

“Tumefanya mazungumzo ya wakati na muhimu juu ya mustakabali wa nchi yetu,” ameongeza.

Mkutano huo unajiri siku chache baada ya Kioni kutangaza kuwa miungano ya vyama vya kisaisa kutoka eneo la Gusii na Mlima Kenya vitaandaa mikutano ya kila wiki kupanga mikakati ya kumnadi Matiangi.

Mbunge huyo wa zamani wa Ndaragwa alifichua kwamba takriban vyama 20 vya kisiasa vinaendeleza mashauriano kabla ya uzinduzi rasmi wa azma ya Matiangi.

Ingawa Matiang’i bado hajatangaza rasmi kuwania kiti cha Urais, anazidi kupata msukumo kuminyana na Rais William Ruto mwaka wa 2027.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here