KIONGOZI WA KANISA ALIYESHAMBULIA MPENZIWE AJISALIMISHA KWA POLISI.

0

Kiongozi wa kanisa na Mfanyabiashara anayedaiwa kumdunga kisu mpenzi wake mara kadhaa amekamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuua.

Elias Mutugi Njeru, mshukiwa mkuu wa jaribio la mauaji ya Florence Wanjiku Gichohi, alijisalimisha pamoja na wakili wake katika kituo cha polisi cha Menengai kaunti ya Nakuru.

“Leo tarehe 25/11/2024, mwanamume mmoja Elias Mutugi Njeru na mshukiwa wa kesi ya jaribio la mauaji ya Florence Wanjiku Gichohi akiwa ameandamana na wakili wake Gakuhi Chege na Associates Advocates waliripoti katika Kituo cha Polisi cha Menengai na kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Nakuru,” Huduma ya Kitaifa ya Polisi imebainisha katika taarifa.

“Amekamatwa na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi wa maafisa wa Kituo cha Polisi cha Menengai.” Imeongeza Huduma ya Polisi.

Kisa hicho kilitokea katika nyumba yao ya kupanga katika Jiji la Nakuru kufuatia mabishano ya kinyumbani ambayo yaliishia katika kudungwa kisu na kujeruhiwa kwa Wanjiku.

Kiongozi huyo katika kanisa moja jijini Nairobi alikuwa mafichoni kwa siku tatu baada ya kisa hicho.

Kanisa ambalo mshukiwa anasemekana kuwa kiongozi lilijitenga na suala hilo huku likitoa wito kwa vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi na kumfikisha mshukiwa mahakamani.

Kisa hicho kimekashifiwa na viongozi kutoka kaunti ya Nakuru wanaotaka Wanjiku kupata haki kwa haraka.

“Tutasimama na familia wakati maafisa wa usalama wanaendeleza uchunguzi. Tutatoa huduma za uwakili bila malipo kwa mwathiriwa,” Katibu Mkuu wa Jinsia Anna Wang’ombe alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here