Mkurungenzi mkuu wa idara upelelezi nchini DCI George Kinoti sasa anamtaka seneta wa Kakamega Cleophas Malala kuomba msamaha kwa madai ya kuiaharibia jina idara hiyo.
Akifika mbele ya kamati ya bunge la seneti kuhusu Usalama, Kinoti aliyeandamana na inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai amesema uchunguzi wao umebaini kuwa madai ya seneta huyo kuwa kikosi maalum cha DCI kilichopewa jina Bravo Zulu Yankee kilitumwa kumuangamiza ni ya uwongo.
Kinoti amesema majina ya watu ambao seneta Malala alidai kuwa ni maafisa wa DCI waliotumwa kumwangamiza si maafisa wake na ni mmoja tu ambaye ni afisa wa polisi mkaazi wa Kakamega anayefanya kazi katika kituo cha polisi cha Thika, kaunti ya Kiambu.