Kelvin Kangethe; Jamaa anayetuhumiwa kumuuwa mpenziwe nchini Marekani kisha kutorokea humu nchini amerejeshwa nchini Marekani.
Mkurugenzi wa mashtaka ya Umaa (DPP) Renson Igonga aliidhinisha kusafirishwa kwake hapo jana akitarajiwa kukafikishwa mahakamani mjini Boston Hapo kesho.
Katika taarifa yake kwa vyumba vya habari, DPP Ingonga amesisitiza ari ya serikali ya Kenya kushirikiana na Marekani kuhakikisha kuwa kesi ya mauaji ya Margret Mbitu inatatuliwa.
“Kwa familia ya marehemu Margaret Mbitu, tunatoa sapoti na maombi,” amesema Igonga.
Mwili wa Mbitu ulipatikana ndani ya gari katika uwanja wa ndege wa Boston akishkiwa kuuwawa na mpenziwe wa zamani Kangethe.
Kangethe alitiwa mbaroni na maafisa wa Interpol akiwa kwenye sehemu moja ya Burudani mtaani Westlands jijini Nairobi.
Hata hivyo, alifanikiwa kutoroka kizuizini kabla ya kutiwa mbaroni tena mwezi Februari mwaka huu