KEVIN KANGETHE ANYIMWA DHAMANA NA MAHAKAMA YA MAREKANI

0
KEVIN KANGETHE
KEVIN KANGETHE

Kevin Kangethe jamaa anayeshukiwa kumuuwa mpenziwe nchini Marekani kisha kutorokea humu nchini amenyimwa dhamana na mahakama ya Boston.

Kangethe alisafirishwa kuelekea Marekani siku ya Jumapili baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Igonga kuidhinisha kusafirishwa kwake.

Waendesha mashtaka wameiambia mahakama kuwa Kangethe alikutana na Marehemu Margret Mbitu, 31, alipokuwa akiondoka kazini eneo la Halifax, Massachusetts usiku wa kuamkia Jumatatu, Oktoba 30, 2023.

“Kati ya kuondoka Halifax na kufika nyumbani kwa Bw. Kangethe huko Lowell, alimshambulia kikatili Bi. Mbitu ndani ya gari kwa kisu,” mwendesha mashtaka Mark Lee aliambia mahakama.

“Kangethe alimuacha na majeraha 10 usoni na shingoni. Masaa 30 baadaye Kangethe aliondoka na mwili wa Mbitu garini mwake na kuelekea uwanja wa ndege wa Logan ambapo aliabiri ndege kuelekea Kenya.” Lee aliongeza.

Kangethe hakukutana na familia ya Mbitu ana kwa ana kwani alijificha kwenye ukumbi wakati wa kesi yake katika Mahakama ya Juu ya Suffolk.

“Tutaendelea kupigana hadi mnyama huyu afungwe na asione mwanga tena,” binamu ya Mbitu, Mary Kinyariro alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here