Kesi ya ufisadi inayomkabili Gavana wa Nairobi Mike Sonko ya ufujaji wa Sh14.1M iliyokuwa ianze kusikilizwa Jumatatu imehairishwa hadi tarehe sita mwezi ujao.
Hakimu Peter Ooko ameagiza kuhairishwa kwa kesi hiyo baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kusema kuwa haikuwa tayari kuendelea na kesi hiyo.
Afisi hiyo imeiambia mahakama kuwa hawangeweza kuendelea na kesi hiyo kwani kesi zingine mbili za ufisadi zinazomkabili Gavana huyo zilikuwa zinaendelea katika mahakama hiyo ya Milimani.
Wakili wa Sonko Cecily Miller hakupinga ombi hilo.