Kesi inayopinga ushauri wa jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge itasikilizwa Novemba 23.
Jopo la majaji watano linatazamiwa kusikiliza kesi hiyo kufuatia mwelekeo uliotolewa Jumatano na jaji wa mahakama kuu James Makau.
Jaji Maraga anatazamiwa kuwakilishwa na wakili James Oduol kwenye kesi hiyo.
Jopo hilo la majaji watano linatazamiwa kuongozwa na Lydia Achode.
Kesi zote zinazohusiana na ushauri huo zimejumlishwa na sasa zitasikilizwa kwa pamoja.
Maraga ambaye ni rais wa mahakama ya upeo alimshauri rais kulivunja bunge baada ya kushindwa kupitisha sheria kuhusu uwakilishi sawa katika nafasi za uongozi.









