Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga wamekaribishwa kwa shangwe na vifijo na wakaazi wa Kisumu walipopelekea kampeini za kupigia debe ripoti ya maridhiano BBI.
Akiwatubia wenyeji waliojitokeza kwa wingi kumkaribisha, rais kwa mara nyingine amewasihi Wakenya kusoma ripoti hiyo kwa makini na kuielewa na kisha kutoa maoni yao.
Kauli za rais Kenyatta zimeungwa mkono na Odinga ambaye amewahimiza Wakenya kusoma ripoti hiyo na kuiunga mkono.
Rais pia ameidhinisha ujenzi wa uwanja wa Jomo Kenyatta unaogharimu Sh415M katika eneo la Nyanza uwanja ambao amesema utakamilika mwaka ujao.
Hayo yakijiri
Baadhi ya wabunge wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya wamepigia debe ripoti hiyo wakisema itataua changamoto ambazo zimekuwa zikilikumba taifa hili ikiwemo ufisadi.
Uhuru atazindua ripoti hio rasmi Jumatatu katika ukumbi wa Bomas.