Kenya yaripoti visa vipya 210 vya corona

0

Mtoto wa miezi sita na ajuza mwenye umri wa miaka 91 ni miongoni mwa watu 210 waliokutwa na corona baada ya kupima sampuli 3,604 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa anasema hii inafikisha 38,378 idadi ya visa vya ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 545,019 tangu kisa cha kwanza kiripotiwe nchini.

Watu 59 zaidi wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 24,740 huku watu 7 zaidi wakifariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 707.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi (55), Kericho (36), Kitui (24), Kiambu (21), Nakuru (19), Mombasa (15), Kisumu (10), Kisii (8), Kilifi (6), Turkana (5), Embu (4), Wajir (2), Machakos, Kakamega, Kwale, Nandi & Kajiado (1).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here