Kenya yaripoti visa vipya 184 vya corona, 7 wakifariki

0

Mtoto wa miezi miwili ni miongoni mwa watu 184 waliopatikana na corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 4,700.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amesema hii inafikisha 38,713 idadi ya visa vya ugonjwa huo hapa nchini kufikia sasa.

Watu wengine 115 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 25,023 huku idadi ya waliofariki ikiongezeka na kufikia 718 baada ya watu 7 zaidi kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 58, Mombasa 22, Kisumu 20, Nakuru 13, Kericho & Trans Nzoia 8, Laikipia & Machakos 7, Uasin Gishu, Narok na Kisii 6, Kiambu & Kwale 4, Homabay 3, Bomet & Embu 2, Pokot Magharibi, Makueni, Nandi & Siaya 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here