Kenya yapigwa jeki katika kuwania nafasi WTO

0

Juhudi za Kenya kuongoza shirika la biashara duniani WTO zimepigwa jeki baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutangaza kumuunga mkono balozi Amina Mohamed anayewania wadhifa huo.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza kuunga Kenya mkono kufuatia ushawishi kutoka kwa rais wa Rwanda Paul Kagame.

Waziri Amina Mohamed ni miongoni mwa watu wengine watano wanaowania nafasi ya kuwa mkurugenzi mkuu wa WTO huku orodha ya mwisho ikitarajiwa kutolewa Jumanne.

Wengine ni Dkt. Ngozi Okonjo (Nigeria) Yoo Myung (Korea Kusini), Mohammad Maziad (Saudi Arabia) na Dkt. Liam Fox (Uingereza).

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here