Kenya yapiga marufuku mikutano ya kisiasa

0

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa siku sitini huku akiwataka viongozi kuonesha mfano mwema kwa kuzingatia masharti ya kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Katika kutangaza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, rais Uhuru Kenyatta amesadiki kwamba wao kama viongozi wamefeli kuonesha uongozi mwema kwani ni wao ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kuongoza mikutano ya hadhara pasipo kuvalia barakoa.

Na sasa ametoa changamoto kwa viongozi kuhakikisha kuwa wamezingatia masharti hayo kwa kusitisha mikutano yao ili kusaidia kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Marufuku hii inajiri siku moja baada ya naibu rais William Ruto kutangaza kuwa amehairisha mikutano yake ya kisiasa kufuatia kuongezeka kwa msambao wa virusi hivyo.

Rais vile vile amesema iwapo kaunti husika itatangaza kuongezeka kwa msambao wa virusi vya ugonjwa huo, basi hatakuwa na budi ila kutangaza kufunga kaunti hizo sawa na kufunga masoko na uchukuzi iwapo taifa litazidi kuandikisha idadi kubwa ya virusi vya ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here