Kenya yakosa kuandikisha maafa ya corona

0

Kwa mara ya kwanza hakujaripotiwa maafa yoyote ya corona nchini Kenya katika muda saa ishirini na nne na hivyo kufanya idadi ya maafa kusalia kuwa 567.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema kuwa watu 241 zaidi wameambukizwa virusi vya corona kwa muda saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 33,630.

Katibu ametangaza pia kuwa idadi ya waliopona imefika 19,434 baada ya watu 66 kupona kutokana na ugonjwa huo.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi inaongoza na visa 113, Mombasa 14, Taita Taveta na Kiambu 10, Kirinyaga na Narok 9, Kajiado 8, Nakuru 7, Turkana 6, Busia na Lamu 5, Trans Nzoia, Kakamega, Kilifi na Kericho 4, Kisumu 3, Makueni ,Nyeri,Machakos na Bomet 2, Embu, Nyandarua na Nandi 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here