KENYA YAKANA KUHUSIKA KATIKA UTEKAJI NYARA WA KIZZA BESIGYE

0

Kenya imekana kuhusika na madai ya kutekwa nyara Na kuondolewa humu nchinii kwa kiongozi wa upinzani wa taifa la Uganda Kizza Besigye.

Katibu wa Masuala ya Kigeni Sing’oei Korir AMESEMA Kenya haina maslahi yoyote ya kibinafsi katika siasa na matukio nchini Uganda.

“Hakuna sababu yoyote kwa Kenya kuwa mshiriki katika kukamatwa kwake,” Korir amesema.

Kauli ya Korir inajiri kufuatia taarifa iliyotolewa na mke wa kiongozi huyo wa upinzani kwamba mumewe alitekwa nyara kutoka kwenye chumba chake mtaani Riverside na kurejeshwa kwa lazma nchini Uganda ambapo kwa sasa anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi.

Besigye alikuwa humu nchini kuhudhuria uzinduzi wa Kitabu cha wasifu wa kigogo wa Upinzani Marha Karua.

“Naiomba serikali ya Uganda kumwachilia mume wangu Dkt Kizza Besigye kutoka anakozuiliwa mara moja. Alitekwa nyara Jumamosi iliyopita alipokuwa Nairobi kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu cha Martha Karua.” Amesema Bi. Bwanyima Besigye kwenye ukurasa wake wa X.

kUTEKWA kwake kunafuatia kisa cha Julai 23 CHA kukamatwa kwa wanaharakati 36 wa Uganda wanaohusishwa naye mjini Kisumu kabla ya kusafirishwa hadi Uganda.

Wanaharakati hao walifunguliwa mashtaka ya uhaini na kupelekwa katika Gereza la Kitalya.

Wanaharakati hao ambao waliachiliwa kwa dhamana hivi majuzi, walikana mashtaka hayo na kusema walikuwa wakihudhuria warsha walipokamatwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here