Kenya yajiunga na Ulimwengu kuadhimisha siku ya kupinga Ufisadi

0

Serikali inajikakamua kuweka mikakati kabambe kuzuia ufisadi katika asasi mbalimbali za serikali.

Hili ndilo hakikisho linalotolewa na rais Uhuru Kenyatta ambaye amesema miongoni mwa mikakati hii ni kuanza kuwafunza wanafunzi maadili mema wanapokuwa shuleni.

Rais Kenyatta amesema haya huku Kenya ikijiunga na mataifa mengine kuadhimisha siku ya kupinga ufisadi.

Na huku rais akitoa hakikisho hilo, tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imesadiki kwamba Kenya iko kwenye mkondo unaofaa katika vita dhidi ya ufisadi.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na Biblia Husema Shajara, Afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak anasema kumaliza ufisadi utachukua muda na utafanikishwa haraka iwapo kila mkenya angeweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Mada kuu ya mwaka huu ni ‘kutwaa kwa maadili’ mali iliyopotea kwa njia za ufisadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here