Kenya yadhibitisha visa vipya 571 vya corona

0

Mtoto wa mwaka mmoja na ajuza mwenye umri wa mia tisini ni miongoni mwa watu 571 waliopatikaa na ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 3,963 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 45,647 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Kwa mara kwanza, kaunti ya Uasin Gishu imeandikisha idadi ya visa 116 sawa na Nairobi ikifuatiwa na Mombasa ambayo imeandikisha visa 74, Kiambu 50, Laikipia 43 na Kericho 41.

Watu wengine 438 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 32,522 huku maafa yakifikia 842 baada ya wagonjwa 3 zaidi kufariki.

Idadi ya wagonjwa walio kwenye vyumbo vya watu mahututi ICU ni 43 huku 41 wakisaidiwa na mashine kupumua. Idadi ya wagonjwa walio katika hospitali mbalimbali ni 1,059 huku wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 2,562.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here