KENYA YADHIBITISHA KISA CHA KWANZA CHA CORONAVIRUS

0

KENYA imedhibitisha kisa cha kwanza cha #Coronavirus.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema mgonjwa huyo na raia wa Kenya aliyesafiri kutoka Marekani kupitia Uingereza.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Kenya alisafiri nchini mnamo Machi 5 ila kwa sasa yuko katika hali nzuri.

Waziri wa afya anasema mwanamke huyo alionesha dalili za kuwa na homa hiyo na alipopimwa alipatikana nayo baada ya kujipeleka hospitalini.

Kwa mujibu wa waziri Kagwe, kwa sasa serikali inawafuatilia watu wote ambao mgonjwa huyo alitangamana nao kubaini hali yao ya kiafya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here