Kenya yaandikisha idadi kubwa ya waliopona corona

0

Kenya imeandikisha idadi kubwa ya waliopona ugonjwa wa corona baada ya watu 4,328 kupona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi hiyo kuwa 31,659.

Kwa mujibu ya waziri wa afya Mutahi Kagwe, watu 4,222 wamepona ugonjwa huo wakiwa nyumbani huku wengine 106 wakipona na kuruhusiwa kuondoka katika hospitali mbalimbali nchini.

Aidha, watu 321 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 3,424 na hivyo kufikisha 39,907 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Nairobi imeandikisha visa 109, Nakuru 37, Trans Nzoia 32, Mombasa 31, Kisumu & Narok 16.

Idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 748 baada ya kufariki kwa wagonjwa 5 zaidi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here