Kenya imeandikisha idadi kubwa ya corona baada ya watu 1,185 kupatikana na ugonjwa huo kati ya sampuli 9,851 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Idadi ya waliofariki inakaribia kufikia alfu moja baada ya watu kumi na saba zaidi kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 53,797 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.
Nairobi inaongoza kwa kuandikisha visa 373, Nakuru 157, Mombasa 118, Kiambu 94 na Kisumu 61.
Idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 981 baada ya wagonjwa 17 zaidi kufariki.
Idadi ya waliopona imefikia 35,876 baada ya watu 272 kupona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Kwa mujibu ya waziri Kagwe, kaunti zinazoshuhudiwa kuongezeka kwa idadi ya visa hivyo ni Kisumu, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi.
Katika kumalizia taarifa yake, waziri Kagwe amewasihi Wakenya kujiokoa na kuokoa taifa lao kutokana na janga hili kwa kutii masharti ya usalama kwani watu zaidi wataambukizwa na tutajipata taabani.