Kenya kupiga jeki vita dhidi ya ugaidi asema rais Uhuru

0

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kwamba Kenya itasalia kuwa katika mstari wa mbele kuongoza juhudi za kupambana na ugaidi katika eneo la Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta ameiambia jamii ya kimataifa katika mkutano kwa njia ya mtandao kwamba hili litaafikiwa kupitia ushirikiano na serikali pamoja na washirika mbalimbali.

Ameongoza kuwa Kenya itatumia ushawishi wake katika baraza la usalama wa umoja wa mataifa kuchangia pakubwa katika kuleta umoja, amani na udhabiti katika kanda hii.

Haya yanajiri saa chache baada ya Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i kutoa orodha ya Wakenya tisa wanaotuhumiwa kufadhili shughuli za kigaidi hapa nchini.

Matiangi ameagiza akaunti za benki za washukiwa hao wanaodaiwa kufadhili shughuli za kundi la kigaidi la Alsha baab kufungwa huku mali zao zikitwaliwa kwa mujibu.

Wakenya hao wanajumuisha Halima Ali, Waleed Zein, Sheikh Boru, Mohammed Ali, Nuseiba Haji, Abdimajit Hassan, Mohammed Ali Abdi, Muktar Ali na Mire Elmi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here