Afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya kusambaza dawa KEMSA Dr. Jonah Mwangi pamoja na wakurugenzi wengine wawili wametumuliwa kwa muda afisini kufuatia madai ya kukiuka sheria za ununuzi na hivyo kusababisha ujujaji wa Sh100b pesa za kukabiliana na janga la corona.
Mwenyekiti bodi ya KEMSA Kembi Gitura anasema Dr. Mwangi ametimuliwa pamoja na mkuu wa idara ya ununuzi Charles Juma na mkurugenzi wa mauzo Eliud Mureithi ili kuiruhusu tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuchunguza madai hayo.
Bodi hiyo imewateua mkuruegnzi wa oparesheni Edward Njuguna kama kaimu afisa mkuu mtendaji, George Walukana kama kaimu mkurugenzi wa mauzo na Edward Buluma kama kaimu mkurugenzi wa ununuzi.
Uchunguzi wa mwanzo wa EACC unaonesha kuwa maafa wa KEMSA walikiuka sheria kwa kutoa zabuni ya moja kwa moja inayogharimu Sh7.7b katika ununuzi wa vifaa vya kupambana na COVID19.