Kaunti zatishia kufunga shughuli na kuwatuma wafanyikazi nyumbani

0

Kaunti zote arobaine na saba zimetishia kufunga shughuli zake tarehe kumi na saba mwezi huu na kuwatuma nyumbani wafanyikazi wote iwapo seneti haitaafikia suluhu la mswada tata wa ugavi wa mapato.

Mwenyekiti wa baraza la Magavana Wycliffe Oparanya anasema hawana budi ila kusitisha shughuli kwani kwa sasa hawana pesa za kuwalipa wafanyikazi wala kuendesha huduma zingine.

Oparanya ametishia kuwa baraza hilo litawasilisha hoja ya kuvunjilia mbali bunge la seneti kwa kukosa kuafikia suluhu la mfumo utakaotumika kugawa shilingi billion 316.

Oparanya ameitaka hazina ya kitaifa kutoa nusu ya mgao wa pesa kwa serikali za kaunti kutumia mfumo wa zamani ili waendelea na huduma.

Sio sisi!

Bunge la seneti nalo limejitetea kuhusiana na madai kuwa kukwama kwa shughuli za kaunti kumechangiwa na maseneta kukosa kupata suluhu la mswada wa ugavi wa mapato.

Kiranja wa wengi katika bunge hilo Irungu Kangata anasema kwa mujibu wa katiba, hazina ya kitaifa inafaa kutoa nusu ya mgao wa fedha kwa serikali za kaunti na hivyo si wao wa kulaumiwa.

Maseneta wamekosa kuafikia suluhu baadhi wakihsinikiza ukubwa wa kaunti kutumika kugawa pesa na wengine kupendekeza idadi ya watu.

Ukosefu wa pesa wachangia migomo

Madaktari katika kaunti ya Kericho wametoa makataa ya siku 14 kushriki mgomo baada ya serikali ya kaunti kukosa kutekeleza mkataba wa maelewano baina yao.

Kupitia kwa muungano wa kutetea maslahi yao KMPDU, madaktari hao wanasema serikali ya kaunti hiyo imekataa kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuongezwa mishahara na kutopandishwa vyeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here