Serikali za kaunti zitasitisha shughuli zake kuanzia Alhamisi hii kufuatia hatua bunge la Seneti kwa mara ya kumi kushindwa kuelewana kuhusu mswada tata wa ugavi wa mapato.
Baraza la magavana kupitia mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya limeziagiza hospitali kutowakubali wagonjwa wa kulazwa huku wafanyikazi wa kaunti wakiagizwa kuchukua likizo ya siku kumi na nne.
Magavana wamechukua hatua hii baada ya kukosa pesa kuendesha shughuli za kawaida ikiwemo kuwalipa wafanyikazi kufuatia mgogoro unaozingira mswada huo wa ugavi wa mapato.
Haya yanajiri siku moja baada ya masenta kukosa kuelewana licha ya rais Uhuru Kenyatta kuahidi kutoa Sh50b zaidi mwaka ujao baada ya kukutana na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya.