Katibu aliyeachishwa kazi na serikali kulipwa fidia ya shilingi moja (Ksh 1)

0

Aliyekuwa katibu katika wizara ya vijana na jinsia Lillian Omollo atalipwa shilingi moja na serikali kwa kumuachisha kazi.

Ndio agizo lake jaji wa mahakama ya Leba Stephen Radido baada ya Omollo kuishtaki serikali kwa kuondoa jina lake kwa orodha ya wafanyikazi wanaopokea mshahara kila mwezi.

Jaji Radido amesema serikali ilikiuka haki za Omollo, lakini kwa sababu alipatikana na hatia ya kujilimbikizia mali kinyume cha sheria katika sakata yashirka la NYS, shilingi hiyo moja inamtosha kama fidia.

Mahakama inaitaka serikali kumlipa Omollo pesa hizo kwa kutofuata sheria wakati ilimuachisha kazi kwani haikumpa notisi.

Tayari Omollo amekata rufaa uamuzi wa mahakama uliompata na hatia katika sakata ya NYS.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here