KALONZO ADAI FERDINAND WAITITU AMEKAMATWA

0
KINARA WA WIPER KALONZO MUSYOKA(KATIKATI)
KALONZO AND WAITITU

Aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu anadaiwa kukamatwa na watu wanaominika kuwa maafisa wa Polisi.

Kinara wa chama cha Wipe Kalonzo Musyoka ametakaidara ya upelelezi wa makosa ya Jinai kutoa taarifa kuelezea kukamtwa kwa Waititu almaarufu “Baba Yao”.

Kukamatwa kwa Waititu kunajiri siku moja tu baada ya Gavana huyo wa zamani kuidhinisha Kalonzo kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao.

“Sisi kama Wakenya kwa kauli Moja tumekubaliana kuwa Kalonzo ndie anaepaswa kuwa Rais mwaka wa 2027,” alisema Waititu katika taarifa ya Pamoja kukemea mauaji na kutekwa nyara kwa wakenya wanaopinga utawala wa Rais William Ruto.

Taarifa hio ilitolewa na Kalonzo, Waititu, kinara wa chama cha Safina Jimmy Wanjigi, Kinara wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa na katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni.

Kalonzo amesema kuwa ataelekea katika makao makuu ya DCI katika Barabara ya Kiambu kusaka majibu kuhusu aliko Waititu.

Matukio hayo yanajiri siku moja tu baada ya mwanabiashara na mwanasiasa Jimmy Wanjigi kudai kuwa watu waliojifunika uso walimwaga damu lita kumi nje ya makazi yake mtaani Muthaiga.

“Walikuja hapa, na unaona damu iliyomwagika nyumbani kwangu. Hawa ni watu ambao wameamua kunitisha tena nyumbani kwangu. Wananiambia watamwaga damu yangu.” Alisema Wanjigi.
Idara ya polisi bado haijatoa taarifa kuhusiana na madai hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here