KALONZO AAPA KUWA DEBENI 2027; ATAKA ODINGA KUMUUNGA MKONO

0
KINARA WA WIPER KALONZO MUSYOKA(KATIKATI)
KALONZO AND WAITITU

Kinara wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo Musyoka amewahakikishia wakenya kuwa atakuwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha urais mwaka 2027.

Akizungumza katika mahojiano na vituo vya radio vinavyopeperusha matangazo kwa lugha ya kiluhya, Kalonzo amesema kuwa ako na uzoefu na anazielewa shida za nchi hii hivyo itakuwa rahisi kwake kushindana na Rais William Ruto katika uchaguzi ujao.

“Nimesubiri kwa miaka 20. Inafika wakati hata dunia inakubali kuwa ni wakati wako,” amesema Kalonzo katika mahojiano hayo.

“Wakati umefika kwa wengine kunifungulia njia ili tuweze kuokoa nchi hii.”
Kalonzo aidha ametaka kinara wa ODM Raila Odinga kustaafu kutoka kwa siasa iwapo atashindwa kutwaa uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC

Akitetea maamuzi yake ya awali ya kuunga mkono Odinga, Kalonzo ameeleza kuwa hayakufanywa kirahisi bali baada ya kutafakari kwa kina na baada ya mashauriano.

“Wengi wameuliza kwa nini niliendelea kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais. Haikuwa ya nasibu-ilitegemea mazungumzo na uchambuzi makini wa matokeo yanayoweza kutokea,” alisema Kalonzo.

Kiongozi huyo wa Upinzani ametaka tume maalum kubuniwa kuchunguza visa vya utekaji nyara ambavyo vimekithiri humu nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here