Jubilee yaitisha mkutano wa dharura na MCAs wa Nairobi

0

Chama cha Jubilee kimewaagiza waakilishi wadi wa Nairobi waliochaguliwa au kuteuliwa na chama hicho kuhudhuria mkutano wa dharura hii leo.

Katika barua, katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju amewataka MCAs hao kufika bila kukosa mwendo was aa sita kujadili masuala ya uongozi wa bunge la kaunti ya Nairobi.

Waakiishi wadi hao wanatazamiwa kujadili uchaguzi wa spika ambao umeratibiwa kufanyika hapo kesho saa nane.

Kiti hicho kilibaki wazi baada ya Beatrice Elachi kujiuzulu huku ikidaiwa kuwa huenda alipata ushawishi wa kungatuka kutoka ikulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here