Jubilee wamkufukuza David Sankok

0

Chama cha Jubilee kimemfukuza mbunge mteule David Sankok kutoka kwa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu uwiano na nafasi sawa.

Spika wa bunge hilo Justine Muturi amedhibitisha kupokea barua kutoka kwa kiranja wa chama hicho bungeni Emmanuel Wangwe ikimuarifu kuhusu uamuzi huo.

Nafasi ya Sankok ambaye ni mwendani wa naibu rais William Ruto inatazamiwa kujazwa chini ya siku kumi na nne zijazo kulingana na kanuni za bunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here