Jubilee wajiondoa katika uchaguzi Msambweni

0

Chama cha Jubilee kimejiondoa kwenye uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Msambweni ambao umeratibiwa kufanyika Disemba 15.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju katika taarifa ametaja maswala mawili muhimu yaliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo.

Kwanza ni ushauri wa jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta alivunje bunge na pili ni kwamba kiti hicho kilikuwa kinashikiliwa na mbunge wa chama cha ODM.

Katika ufafanuzi wake, Tuju amesema maswala haya ni muhimu kwa taifa na yanahitaji ushauriano na ushirikiano wa kisiasa kuyatatua.

Naibu rais William Ruto amesema amekubaliana na uamuzi huo licha ya kwamba alikuwa na maoni tofauti.

Haya yanajiri siku moja baada ya Mariam Sharlet anakimezea mate kiti hicho kukigura chama cha ODM na kujiunga na Jubilee akiwa na matumaini kwamba angepewa tiketi ya kuwania wadhifa huo.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge Suleiman Ramadhan Dori mnamo mwezi Machi mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here