Je, rais ataondoa kafyuu?

0

Je, rais Uhuru Kenyatta atalegeza au kukaza kamba kwenye masharti ya kupambana corona?

Swali hili litapata majibu Jumanne wiki ijayo wakati rais atalihutubia taifa.

Kafyuu ya kutotoka nje kati ya saa tatu usiku na saa kumi asubuhi itasalia kuwepo hadi siku hiyo ambayo ni Septemba 29 wakati rais atawafahamisha Wakenya kuhusu iwapo mikakati iliyopo itasalia au itaondolewa kufuatia kuendelea kupungua kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo.

Taarifa kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua imearifu kuwa hotuba hiyo ya kumi na mbili ya rais iattoa mwongozo kwa taifa kuhusu hatua zitakazofuatwa katika kupungua msambao wa virusi hivyo.

Hotuba hiyo itakuja siku moja baada ya mkutano wa kamati ya kitaifa Jumatatu kujadili hali ya msambao wa virusi hivyo chini ya uongozi wake rais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here