Jamii za Shona na Wanubi zataka kutambuliwa

0

Tume ya kutetea haki za kibinadamu (KHRC) imeitaka serikali ya Kenya kuwatambua na kuwapa uraia watu kutoka jamii tengwa ya Shona ili kuwawezesha kuishi kama Wakenya wengine.

KHRC inasema watu kutoka jamii hiyo wanaendelea kuishi kwa umasikini kwani wameshindwa kupata stakabadhi muhimu za serikali kama vile vyeti vya kumiliki ardhi kwani hawana vitambulisho.

Jamii ya Shona iliingia nchini Kenya kutoka Zimbabwe zaidi ya miaka hamsini iliyopita na hadi leo hawajatambuliwa.

Wakati uo huo

Jamii ya wanubi ambao wanaishi mtaani Kibra, Nairobi imetishia kuenda mahakamani iwapo  serikali haitashughulikia malalamishi ya wao kutambulika kama wakenya.

Mwenyekiti shirika la kutetea haki zao (Nubian Rights Forum) Shafi Ali, anasema licha ya kuwa na kikao na waziri wa usalama ya ndani Dr Fred Matiang’i, serikali imekosa kutekeleza baadhi ya masuala waliyokubaliana ikiwemo kuwazesha vijana kupata vitambulisho vya kitaifa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here