‘James Bond’ wa Bungoma afariki

0

Mwanaume aliyegonga vichwa vya habari kutoka kaunti ya Bungoma mwaka 2016 kwa kudandia helikopta amefariki.

Sale Wanjala aliyepewa jina la utani ‘James Bond’ amefariki akiwa na umri wa miaka 36 katika hospitali ya rufaa ya Bungoma.

Familia yake inasema mwendazake amekuwa mgonjwa kwa muda na alifariki punde baada ya kufikishwa hospitalini.

‘Bond’ alidandia ndege iliyokuwa imebeba mwili wa mfanyibiashara Jacob Juma kwa mazishi.

Mwendazake alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kuhatarisha maisha yake lakini akawachiliwa baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here