Jamaa amkata mwenzake mkono kwa sababu ya deni la Sh150 Migori

0

Mwanamme mmoja amelazwa katika hospitali ya Rapcom huko Awendo, kaunti ya Migori baada ya mkono wake kukatwa kwa panga kufuatia mzozo wa deni la Sh150.

Inaarifiwa kuwa mwathiriwa Maurice Ouma alishambuliwa na Josiah Agutu baada ya kugombania deni hilo lililobaki baada ya kumuuzia simu ya Sh700.

Joy Christine, mkewe Agutu anasema mumewe alikataa kulipa pesa hizo zilizosalia na hivyo Ouma akamshambulia kwa panga.

Naibu mkuu wa Polisi Awendo Jacob Waluhu anasema mshukiwa alikamatwa katika eneo la Lolgorian, kaunti ya Narok alikokuwa ameenda kujificha baada ya kumkata mwenzake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here