Jaji mwingine ajiondoa kwenye kesi ya Sonko

0

Nzioki Wa Makau amekuwa jaji wa pili kujiondoa kwenye kesi ambapo gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko anataka mahakama kuzuia kuendelea kwa mjadala wa kumuondoa mamlakani.

Jaji Makau amesema amejiondoa kwenye kesi hiyo kwa misingi kwamba wakili wa bunge la kaunti ya Nairobi Ndegwa Njiru aliwasilisha ombi la kumtaka kujiondoa kwenye kesi hiyo kufuatia madai ya mapendeleo.

Wakili huyo alidai kuwa jaji Makau alikuwa amepokea hongo ya Sh7M kutoka kwa Sonko ili kutoa maamuzi yanayompendelea.

Itakumbukwa kwamba jaji James Rika alijitoa kwenye kesi hiyo juma lililopita baada ya wakili wa Sonko Harrison Kinyanjui kumtuhumu kwa mapendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here