Magavana wanalia kwamba hawana pesa za kuwawezesha kupambana vilivyo na janga la corona.

Kupitia kwa mwenyekiti wake wa afya Profesa Anyang Nyong’o, baraza la magavana linalalama kwamba serikali kuu haijawatumia mgao wa mwezi Machi na Aprili na hivyo kuwafanya kukopa ili kuendesha shughuli za kawaida.

Baraza hilo vile vile limewaonya Wakenya dhidi ya kuendelea kukaidi masharti ya usalama ikiwemo kwenye magari ya uchukuzi wa umma na kuendelea kuhudhuria matanga licha ya kukatazwa.

Kwa sasa Kenya imedhibitisha visa 156,981 vya corona huku maambukizi ya ugonjwa huo nchini yakiwa katika asilimia 10%.