Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) mwaka huu kufikia tarehe kumi mwezi ujao wa Mei.

Haya ni kulingana na waziri wa elimu Profesa George Magoha ambaye amesema mtihani huo uliokamilika hii leo umekuwa na mafanikio ya asilimia 99.9 licha ya changamoto za kuwepo kwa corona nchini.

Hata hivyo Profesa Magoha ameongeza majina ya wasimamizi wa mtihani 27 yamewasilishwa kwa tume ya walimu nchini(TSC) kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuhusika katika majaribio ya kufichua mtihani huo kabla ya wakati wake kamili.

Zaidi ya watahaniwa laki saba kote nchini walikalia mtihani huo.